William T. Stanley
Bill Stanley anafanya kazi Field Museum of Natural History in Chicago, U.S.A lakini kila mwaka anafanya utafiti juu ya mamalia wadogo wa Tanzania kwa miezi mitatu. Iwapo unapenda mamalia wa Tanzania, angalia orodha yao kwenye tovuti www.fieldmuseum.org/tanzania.
|
Rebecca Banasiak
Rebecca Banasiak ndiye mtaalamu wa kuandaa vifaa kama mabango, kalenda na vijarida vinavyotumika katika kutoa elimu inayolenga mamalia wa Tanzania. Amefanya kazi hii kwa miaka kadhaa na anapendelea kufanya kazi za sanaa anapokuwa na muda wa mapumziko.
|
Kim M. Howell
Profesa Kim M. Howell amekuwa akifundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tangu mwaka 1970 katika Idara ya Wanyama na Uhifadhi wa Wanyamapori. Anajishughulisha na maswala mbalimbali ya ikolojia na maeneo wanapoishi mamalia wadogo, ndege, nyoka na vyura. Amechapisha makala nyingi kwenye majarida ya kitaaluma na vitabu kadhaa. Utafiti wake kwenye maeneo yenye utajiri mkubwa wa bioanuai yanayotishiwa kutoweka (biodiversity hotspot) nchini Tanzania umevumbua spishi mpya za virukanjia na vyura.
|
Philip Kihaule
Mzee Philip Kihaule alifanya kazi kwa miaka mingi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo alikuwa fundi wa kisayansi (scientific technician) katika Idara ya Wanyama. Kabla ya hapo alifanya kazi katika nyanja ya tiba akishughulikia wadudu (medical entomology) kwenye maeneo mengi ya Tanzania. Ingawa amestaafu, utaalam wake umemfanya awe na kazi nyingi za utafiti juu ya mamalia kuliko wakati mwingine wowote.
|
Maiko Munisi
Maiko Munisi ni mkazi wa Amani, Tanga na ni mshiriki muhimu wa miradi mbalimbali ya bioanuwai. Mbali na mradi wa mamalia wa muda mrefu, Maiko anafanya utafiti juu ya vyura na ndege wa Milima ya Tao la Mashariki, na ameshiriki pia katika miradi ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
|
Mary Anne Rogers
Mary Anne amefanya utafiti katika mazingira mbalimbali ya Tanzania na alikuwemo kwenye timu iliyofanya utafiti wa kwanza wa mamalia wadogo wa Kilimanjaro. Mwaka 2005, Mary Anne alivumbua spishi mpya ya Congosorex, kwenye Milima ya Udzungwa. Uvumbuzi huu ulikuwa muhimu na ulibadilisha jinsi tunavyoelewa mahusiano ya kihistoria ya mfumo huo wa milima.
|
|
Imani N. Swilla
Imani Swilla ni Profesa Mshiriki Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Anafundisha Kifaransa, Tafsiri na Isimu jamii. Aidha, ana uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika tafsiri na ukalimani wa mikutano kwa kutumia lugha za Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili.
|